Molangu nipe rehema,
hadithi njema nitunge,
wanelimu wakisoma,
iwamulike ja nwenge,
iwaonyeshe hekima
na akili iwajenge,
wasome watafakari,
wafate yalo adili
na iwajaze karama,
ili haki waichunge,
watawale kwa huruma,
na dhuluma wajitenge,
wamkumbuke Rahima,
ashirari wajikinge,
wasome watafakari,
wafate yalo adili.
Leave a Reply