Lila na Fila Havitangamani

October 24, 2023

Ewe mkubwa wa miungu,
Enyi mizimu ya babetu,
Enyi watawala wa mbingu,
Mwafahamu walimwengu,
Kuwa naomba salama.

mimi nimetoa fungu,
Fungu la nyama na mbegu,
Vimechanganywa na dengu,
naomba nitoe pingu,
Ili nipate usalama.

Pia na nyinyi wazazi wangu,
mliotoweka, nawaomba usalama
nimepiga magoti mbele yenu
kwa moyo wa unyenyekevu,
nikiwatolea sadaka zangu hizi,
nikiwaomba usalama.

Comments 0

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *